Amos 1:13-15

13 aHili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Amoni,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi
ili kuongeza mipaka yake.

14 bNitatuma moto kwenye kuta za Raba
ambao utateketeza ngome zake
katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano,
katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba.

15 cMfalme wake atakwenda uhamishoni,
yeye pamoja na maafisa wake,”
asema Bwana.
Copyright information for SwhKC